MWANAMUZIKI Mnigeria ambaye amekuwa kinara wa kunyakuwa tuzo katika tasnia ya sanaa, D’Banj amepata tuzo ya Entertainment Icon Award 2016 inayotolewa na Black Entertainment Film Fashion Television and Arts (BEFFTA) aliyokabidhiwa na Lord John Bird kwenye ndani ya Bunge la Mabwanyenye (Matajiri) huko Westminster, London nchini Uingereza.
D’Banj (kushoto) Lord John Bird
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Dr. Pauline Long (Mwanzilishi wa BEFFTA Awards), Chief Bimbo Afolayan ambaye ni mwenyekiti wa BEFFTA, Dayo Olomu na wengine wengi.
Yesterday, I received the #BEFFTA Entertainment Icon Award at the British House of Parliament, From Lord John Bird. I’m Humbled ! Oossshee pic.twitter.com/b6HbdeqRha
— D’banj D Kokomaster (@iamdbanj) November 11, 2016



