×

Baada ya Miaka 56 Akiwa Amecheza Filamu 200, Jackie Chan Anyakuwa Tuzo ya Oscar

jackie-chan-awards

MWIGIZAJI maarufu duniani wa michezo ya Kung-Fu, Karete na vichekesho, Jackie Chan ameshinda Tuzo ya Oscar ikiwa ni miaka 56 tangu aanze kucheza filamu.

jackie-chan-win-awardsMzaliwa huyo wa Hong Kong, China mwenye kipaji kikubwa kwenye tasnia hiyo ametunukiwa tuzo ya Heshima ya Oscar ambayo ni moja kati ya tuzo kubwa kabisa duniani akiwa tayari amecheza filamu zaidi ya 200 tangu aanze kazi hiyo.

jackie-chan-win-oscar-awardsJackie Chan aliyeanza uigizaji wa filamu mwaka 1960, alitunukiwa tuzo hiyo Jumamosi iliyopita, November 2016 na kuungana na mastaa kibao waliotangulia ambao walishawahi kutunukiwa tuzo hizo.

jackie-chan-governors-awardMwigizaji mwenzake kwenye filamu ya Rush Hour, Tom Hanks, Michelle Yeoh waliungana naye stejini na kuwatambulisha kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo.

jackie-chan-win-oscarsWakati akitoa neno la shukrani, Bwana Chan aliwashukuru mashabiki wote kwa kuwao ndiyo wamemfanya aendelee kutengeneza filamu bora zaidi ili kukidhi kile wanachokihitaji.