KUIDHINISHWA kwa Bodi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kuweka mabilioni ya fedha katika benki binafsi ndiyo sababu iliyomfanya Rais John Magufuli kuivunja bodi hiyo.
Rais Magufuli aliyasema hayo leo katika sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria huko Kibaha Mkoa wa Pwani aliposisitiza kwamba TRA walichukua mabilioni ya fedha na kuyaweka kwenye akaunti za muda maalum (fixed accounts) katika benki nane ambapo bodi ikaidhinisha.
Wiki iliyopita Rais Magufuli alivunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu bila kueleza sababu zozote.


