DAR ES SALAAM: NI baada ya Diamond kuibuka kwenye interview ya Kipindi cha XXL cha Clouds Fm na kueleza mengi ikiwemo bifu lake na msanii mwenzake Ommy Dimpoz amekuwa akipiga simu kuomba wauzngumze wamalize bifu lao.
Baadhi ya mambo aliyoyazungumza Diamond “Dimpoz kashatuma watu wengi kuomba msamaha, kashamtuma Salam. Alishanipigia mpaka simu, sikupokea, sasa ningezungumza nini?”
Hizi ni Sentensi 32 Za Diamond Platnumz Alipohojiwa na Clouds FM, Amfungukia Wema
Jambo ambalo lilimuumiza Dimpoz akaandika kwenye twitter kuwa Meneja wa Diamond, Sallam ndiye amekuwa akimpigia Dimpoz ili waongee kuyamaliza, aliamua kuomba interview kwenye kipindi hico hicho cha radio akafunguka haya jana.
“Baada ya choko choko zote, nilipo ‘shoot’ video ya Wanjera na kumuweka Wema (Wema Sepetu) ndio balaa lilipoanzia hapo.
“Mimi sikumweka Wema Sepetu kwenye wimbo wangu kwa makusudi, lakini ana amashabiki wengi na niliona hii itanisaidia.
“Wema ni rafiki yangu kitambo kabla hajaanza uhusiano na Diamond. Na walivyo-‘kiss’ mara ya kwanza kwenye gari nilikuwepo.
Ommy Dimpoz: Nilivurugana na Diamond Kisa Wema Sepetu, Aanika Bifu la Kiba na Diamond
Sinema ikaendelea tena baada ya Dimpoz kufunguka hayo yote, Diamond akajibu kwa mara nyingine kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Majibu hayo yamechukuliwa kama mastaa hawa sasa ni kama wanatafuta sifa kwa mashabiki.
Ameandika:
Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi…. Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???😟 hii nayo ni #KOKORO ujue.
EXCLUSIVE: Ommy Dimpoz Akizungumzia Beef yake na Diamond

