×

Ummy Apokea Vifaa vya Macho Kutoka Standard Chartered

1Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered,  Sanjay Rughni (kushoto) akisoma hotuba kwa waziri Mwalimu.

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, leo amepokea vifaa vya tiba ya macho kutoka Benki ya Standard Chartered ili kuisaidia serikali kutoa huduma katika hospitali mbalimbali.

2Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza katika hafla hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,  Sanjay Rughni,  amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia  wagonjwa mbalimbali wanaokwenda hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu, ambapo miongoni mwa hospitali zitakazonufaika ni  za Mkoa wa Dar es Salaam na rufaa za mikoani.

3

Sanjay Rughni (kushoto katikati) akimkabidhi waziri Mwalimu moja ya vifaa vya tiba ya macho.

4Baadhi ya vifaa vya macho vilivyokabidhiwa.

5Moja ya vifaa vilivyotolewa na benki hiyo.

Na Denis Mtima/Gpl