STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amezua sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii baada ya jana Jumanne kupost kwenye akaunti yake ya Instagram selfie akiwa amevalia boxer nyeusi tena bila aibu.Mkali huyo ambaye anatamba kwa sasa na ngoma ya ‘Salome‘ aliyofanya cover ya Saida Karoli, kwenye picha hiyo,
aliandika:
Straight from the Changing room!…I think i need to go back to the gym so that i can be more flexible on m 24th Pre-XMass Parformance in Dar Es Salaam.
Mbali na kufunika kwa emoji kwenye eneo la sehemu zake za siri, selfie hiyo imezua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wake huku wengi wakimponda staa huyo kwa kukosa staha na kujiaibisha mwenyewe kwa jamii na kwa viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakienda ofisini kwake (WCB) kumtembelea.
POST YENYEWE HII HAPA