Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC keshokutwa Jumamosi watamuaga beki wao kiraka ambaye ni raia wa Rwanda, Mbuyu Twite.
Twite aliyetua klabuni hapo mwaka 2012 anaondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na ataagwa rasmi kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU kutoka Zanzibar Jumamosi ya Juni 10, 2016.

Mchezo huo wa kirafiki utapigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na utaanza saa 10 kamili jioni.
Uongozi wa klabu ya Yanga umebainisha viingilio vya mtanange huo kuwa ni shilingi 5,000/ kwa mzunguko na shilingi 10,000/= kwa VIP huku ukiongeza kuwa tiketi za mchezo huu zitakuwa ni za kielectroniki kwa kadi za Selcom.

