×

Wakati Wizkid Akitajwa Tuzo za Grammy 2017, Davido Atimkia Chuo

davido-2NIGERIA: Staa wa ngoma ya Skelew iliyotamba kuanzia mwaka 2013, Mnigeria David Adeleke aka Davido amesema hivi karibuni anataria kurudi chuoni kusoma ili kuweza kujiimarisha zaidi kieleimu.

Uamuzi huo wa Davido umekuja siku chache baada ya mpinzani wake kwenye tasnia ya muziki nchini humo, Wizkid kuchaguliwa kuwania Tuzo za Grammy 2017 ambazo hutolewa kila mwaka nchini Marekani.

WizkidWizkid

Davido ameeleza kuwa hivi karibuni atarudi kwenye Chuo Kikuu cha Babcock kusoma Shahada ya Udhamili ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) ili aweze kujiweka sawa kielimu.

mkali huyo mwenye umri wa miaka 24 anatazamiwa kujipanga na kujiandaa kupambana vilivyo na mpinzani wake, Wizkid aliyekacha masomo kwenye Chuo Kikuu cha Lead City na kuingia kujikita kwenye muziki ambao kwa sasa umampa manufaa makubwa.

Wizkid ambaye ni bingwa wa pop kwa sasa Afrika, katika Kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikishwa, ameteuliwa kuwania tuzo hizo kupitia wimbo alioshirikishwa Drake wa ‘One Dance’ ambamo pia ameshirikishwa rapa Mfilipino Kyla unaopatikana kwenye Albamu iitwayo Views.

Albamu ya Drake aliyoiachiwa Aprili 2016 ‘Views’ imechaguliwa kuwania Kipengele cha Albamu ya Mwaka ikichuan na Adele (’25’), Justin Bieber (‘Purpose’), Sturgill Simpson (‘A Sailor’s Guide To Earth’), na Beyonce (Lemonade).

halotel-strip-1-1

WALICHOKISEMA BARAZA LA SANAA JUU YA WANAOTAKA KUTOA TUZO