PWANI: Serikali ya China imetoa ufadhili wa ujenzi wa uwanja wa Michezo kwa Shule ya Msingi Msoga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambako ndiko alikozaliwa rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza katika hafla ya kuoneshwa eneo patakapojengwa uwanja huo Rais mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ameishukuru Serikali ya China kwa msaada huo kwa kuwa michezo ni kitu muhimu kwa watoto huku akitoa rai kwa Halmashauri ya Chalinze kulinda eneo hilo.
Kwaupande wake Mwakilishi wa Balozi wa China amesema kuwa China inajivunia uhusiano mwema uliopo kati ya China na Tanzania, na watahakikisha wanajenga uwanja huo kwa wakati ili kuwapa fursa watoto kufurahia michezo.
Nae Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametoa rai kwa wananchi wake kuhakikisha eneo lililotengwa linalindwa ili dhamira ya China kujenga uwanja huo itimie



