×

Mapya Yaibuka Kufuatia Miili 6 Kufungwa Kwenye Viroba na Kutupwa Mto Ruvu (Picha+Video)

ruvu-1 ruvu-2

Mto Ruvu ambapo miili sita ya watu ilikutwa ikielea mnamo Desemba 6, 2016.

ruvu-5

Mojawapo ya kaburi ilipozikwa baadhi ya miili.

ruvu-3

Mkazi wa Kitongoji cha Mtoni akiwaonyesha wanahabari wetu (hawapo pichani) ilipookotwa miili ya watu sita ikielea.

ruvu-4

Mkazi huyo akimwelekeza mwanahabari wetu ilipozikwa miili mingine.

ruvu-6

…Hapa akiwapeleka wanahabari wetu eneo ilipozikwa miili mingine.

ruvu-7

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mtoni, Maneno Mafumba wakati akihojiwa na mwanahabari wetu.

ruvu-8

Maneno Mafumba akiwaelezea kwa undani wanahabari wetu kuhusu tukio hilo.

ruvu-9

Mwananchi wa eneo hilo akinawa katika maji ya mto Ruvu ilipokutwa miili ya watu sita.

ruvu-10

Mashine zinazovuta maji kutoka mtoni kupeleka kwa wananchi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

ruvu-11

ruvu-12

Wakazi wa Kitongoji cha Mtoni wakichukua maji yanayotoka Mto Ruvu kwa matumizi mbalimbali.

KUFUATIA sakata la miili sita ambayo haikutambulika kukutwa ikielea katika Mto Ruvu eneo la Bagamoyo, Mkoa wa Pwani mnamo Desemba 6, mwaka huu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba, huku ikiwa imeharibika vibaya mapya yameibuka.

Kikosi kazi cha Global TV Online kimeamua kutimba mpaka eneo hilo la tukio ili kujua kwa undani ni nini kilichopelekea miili hiyo kukutwa ikielea kwenye mto huo na hatua gani zimechukuliwa mpaka sasa.

Wakazi wa eneo la Kitongoji cha Mtoni, Kata ya Makurunge, wilayani Bagamoyo wakiongea na Global TV Online wamesema baada ya kugundua miili hiyo ikielea katika Mto Ruvu, walimpigia simu Mwenyekiti wao wa Kitongoji cha Mtoni, Maneno Mafumba ambaye alifika kujionea tukio hilo.

Bwana Maneno baada ya kufika naye alimpigia simu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bagamoyo, OCD Maro, aliyefika eneo hilo akiambatana na madaktari wa Hospitali ya Bagamoyo kisha wakaiopoa miili hiyo kabla ya kuizika kutokana na kuharibika vibaya.

“Mnao tarehe 6, Desemba mwaka huu nilipigiwa simu na raia wema na kuambiwa kuwa huku kwenye mto tunaona viroba vinaelea lakini hatujui ndani yake kuna nini njoo tuviangalie, nilipofika tukavisogeza pembeni na kukuta baadhi ya miguu imejitokeza kwa nje nikapiga simu kwa OCD aliyekuja na polisi pamoja na madaktari tukaamua kuvifungua na kujiridhisha kuwa kweli ni miili ya binadamu hivyo tukaamua kuizika kutokana na kuharibika vibaya.” Alisema Maneno

Aidha Maneno anasema mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kupotelewa na ndugu yake hadi sasa katika maeneo hayo hata yaliyo karibu na Bagamoyo.

Global TV iliamua kufunga safari hadi kwa OCD Maro, ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo japo bado hajui wapi ilipotokea na kusema uchunguzi bado unaendelea.

“Ni kweli miili hiyo ilikutwa ikielea na tuliiopoa pamoja na madaktari kwa msaada wa wananchi na tuliamua kuizika kufuatia kuharibika vibaya baada ya kuifanyia uchunguzi wa madaktari na kama miili ingekuwa haijaharibika vibaya ingehifadhiwa mochwari kwa ajili ya utambuzi.” Alisema OCD Maro

Mbali na ufafanuzi huo, OCD Maro aliwataka wanahabari wa Global TV kufika kwa RPC wa Pwani, ACP Mshongi kwa taarifa zaidi maaana yeye ndiye msemaji mkuu wa mkoa.

Global TV Online ilimtafuta RPC Mshongi ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo lakini akasema muda huo alikuwa safarini kuelekea wilayani Mkuranga.

Katika mahojiano ya Global TV na wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa wamekumbwa na taharuki kufuatia tukio hilo la kusikitisha, wamelaani kitendo hicho ambacho wanasema kimewatia hofu maana hadi sasa hawajui kama mauaji hayo yamefanyika katika kitongoji chao ama la.

majaliwa

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Baraza la Maulid lililofanyika  kitaifa, Shelui, Singida jana.

Kuonyesha kuwa bado taarifa sahii kuhusu tukio hio hazijapatikana, jana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa mgeni rasmi kwenye Sikukuu ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambayo kitaifa ilifanyika Shelui, Iramba mkoani Singida baada ya kuona kutatizwa na tukio hilo, alitoa muongozo kwa Waziri Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya ulinzi na usalama nchini kuhakikisha anafanya uchunguzi wa kina kuhusu miili hiyo.

Kabla ya muongozo wa Waziri Mkuu, Waziri Nchemba akihojiwa na kituo kimoja cha runinga jana asubuhi alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa miili hiyo ilikuwa ni ya wahamiaji haramu, walioingia nchini kinyume na sheria lakini hakufafanua zaidi.

ITAZAME VIDEO YA TUKIO HILO HAPA;

Picha / Video: Richard Bukos na Issa Mnally / GPL

halotel-strip-1-1