×

Breaking News: Mbuge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Apata Ajali, Mtoto Afariki Kwenye Ajali Hiyo

Sugu

MBEYA: Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV leo Desemba 17, 2016 zinasema kuwa Mbunge wa Jimbo loa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto  ’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.

Mhe. Mbilinyi alikuwa akielekea uwanja wa ndege Songwe ndipo alipo fika maeeneo ya Iyunga akapata ajali hiyo mbaya japo yeye na dereva wake, Gabriel Andrew (43) hawajapata madhara yeyote mpaka gari hilo lilipo weza kusimama eneo la Tazara Mbeya.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne kati ya sita wamejeruhiwa baada ya kupata ajali kwa gari lao kupinduka wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi  ‘Sugu’. Askari Polisi hao wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, wakatibiwa na wameruhuaiwa kuondoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo nja kwamba dereva wa gari hilo, Gabriel Andrew anashikiliwa na Jeshi la  Polisi mkoani humo.

NILIPIGWA NA MGAMBO NIKAPOTEZA MTAJI WANGU, MAKONDA NISAIDIE MAISHA MAGUMU