×

Mambo mawili ya kumtoa machozi Sanchi

sanchoka-2Na Imelda Mtema, Gazeti la Ijumaa

Mwanamitindo ambaye hivi karibuni amekuwa gumzo kutokana na umbo lake, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefungukia mambo mawili ambayo kila akiyakumbuka hujikuta akibubujikwa na machozi.

sanchoka_web48Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni juu ya maisha yake kwa sasa, Sanchi ambaye awali alikuwa akifahamika kwa jina la Sanchoka alisema kuwa, anajisikia furaha kutokana na jamii inavyomjadili na kusema kwamba, huenda amepewa umbo alilonalo kwa makusudi.

sanchoka_web41-1“Nina furaha na maisha yangu, najua kuna baadhi wanakwazika na life style yangu lakini mimi niko poa,” alisema Sanchi na kuongeza:

“Ila kuna wakati huwa nalia ninapokumbuka baadhi ya matukio ambayo yaliniumiza sana. Kwanza nakumbuka nikiwa na umri wa miaka sita, nilinusurika kubakwa na rafiki wa mjomba wangu. Nisingependa kulizungumzia sana hili kwa kweli.

“Pia huwa nalia sana nikimkumbuka marehemu baba yangu. Miaka 14 imepita tangu baba yangu afariki lakini bado siamini kama siko naye. Alikuwa akinipenda sana lakini Mungu akampenda zaidi,” alisema Sanchi.