×

Wanamuziki Waliovuma 2016

darassa-muziki

Darassa

Alianza kuvuma zaidi kuanzia Januari alipoibuka na Wimbo wa Kama Utanipenda kisha akatoa Heya Haye na Too Much. Kwa sasa Wimbo wa Muziki umemfanya azidi kung’ara.

kiba-newKiba

Mwaka huu, amevuma tena hasa alipotoa Wimbo wa Aje. Ameshiriki tuzo nyingi zikiwemo, HiPipo (Uganda), AFRIMA (Nigeria), MTV EMA (Uholanzi) pamoja na EATV (Tanzania).

man-fongoMan Fongo

Alianza kuvuma kuanzia Juni alipoibuka na Wimbo wa Hainaga Ushemeji uliokuwa na mahadhi ya Singeli. Kuibuka kwake kukaupa hai muziki huo na kuwafanya vijana wengi nao kuibuka.

jideJide

Wimbo wa Ndi Ndi Ndi uliotoka Machi mwaka huu umemfanya kuvuma na kumpa shoo nyingi kupitia ziara yake ya Naamka Tena. Bado anaendelea kuvuma na Wimbo wa Sawa na Wao.

Bella

Tangu atoa nyimbo zake zikiwemo Nagharamia, Nani Kama Mama. Bella bado anaendelea kuvuma hadi sasa. Licha ya kuachia Wimbo wa Nishike, amekuwa miongoni mwa wasanii wanaoendelea kupiga shoo za pesa ndefu.

Navy Kenzo

Wawili hawa wanaounda kundi hili, Aika na Nahreel wameendelea kuvuma hasa mwezi Juni walipotoa Wimbo wa Kamatia. Wamelamba mikataba kibao.

Raymond

Ni zao kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Amevuma kupitia Wimbo wa Kwetu na Natafuta Kiki na Salome alioshirikiana na Diamond.

FA

Alivuma kuanzia mwezi Juni alipofunga ndoa na mzazi mwenzake anayefahamika kwa jina la Helga. Kwa sasa anaendelea kuvuma zaidi kupitia Wimbo wa Dume Suruali.

Vanessa

Amezidi kujihakikishia kuwa ni miongoni mwa mastaa wa kike wa Muziki wa Bongo Fleva wanaoutambulisha kimataifa. Kwa mwaka huu ameshiriki tuzo nyingi za kitaifa na kimataifa zikiwemo HiPipo (Uganda), Soundcity (Nigeria), NEA (Nigeria), MTV Africa (MAMA), (Afrika Kusini) na EATV (Tanzania).

Diamond

Ameendelea kuvuma tena mwaka huu. Licha ya kumsainisha msanii Rich Mavoko katika lebo yake ya WCB ameendelea kutikisa kwenye nyimbo zake ikiwemo Kidogo akiwa na P-Square, Salome akiwa na Raymond. Ameshiriki katika tuzo nyingi za kitaifa pamoja na kupataza ziara na wasanii wakubwa nchini Marekani akiwemo, Ne-Yo.