×

Mkesha wa Krismasi Leo, Jahazi Kuwasha ‘Moto’ Dar Live

jahazi2BAADA ya kusubiriwa kwa muda mrefu, hatimaye imefika ambapo leo (Mkesha wa Krismasi) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kutakuwa na bonge la shoo litakalowahusisha Kundi la Muziki wa Taarab, Jahazi Modern na mkali wa Singeli, Msaga Sumu.

Itakuwaje?

jahaziiiAkizungumzia usiku huo, Meneja wa Dar Live na Jahazi, Juma Mbizo alifunguka miongoni mwa vitu vitakavyofanywa na Jahazi leo kuwa, kwa mara ya kwanza watawashusha wakali wawili, mkongwe wa kupiga kinanda, Ally Jay pamoja na dada mwenye sauti adimu, Mosi Suleiman.

“Shoo nzima itaanza saa mbili usiku kwa kiingilio cha shilingi 7,000 tu. Kutakuwa na redcarpet ambayo kila atakayekuja atapata fursa ya kupiga picha na mastaa kibao watakaokuwepo.

wpid-3001“Pia mashabiki wa burudani watapata kuishuhudia Jahazi inayoongozwa na vichwa vikali kama Leila Rashid na Amigo ambapo niseme tu usiku huo wataporomosha nyimbo zao zote kali kuanzia Tiba ya Mapenzi, Nina Moyo Sina Jiwe, Nilijua, Mpenzi Chocolate na nyingine nyingi wakisindikizwa na mkali wa Singeli,” alisema Mbizo na kuongeza kitu kingine waje washuhudie sapraizi watakayoifanya Jahazi ambayo haijawahi kutokea katika kundi hilo tangu kuanzishwa.

jahazi-fatma-mahmoudKrismasi ya kesho sasa!

Mbizo aliongelea pia shoo itakayofanyika kesho katika Sikukuu ya Krismasi kuwa, Dar Live itawashusha marapa wa Muziki wa Dansi wanao-kubalika zaidi ya 10 kati ya 27.

“Marapa hao wanatoka bendi kubwa na kongwe kama T.O.T, FM Academia, Twanga Pepeta na nyingine kibao. Listi kamili ya marapa hao ni Chokoraa, Papy Cataloge, Seven, Toto Kalala, Mirinda Nyeusi, Fagason, Kaba5, Kitokololo, Hilter na Sauti ya Radi,” alisema Mbizo na kuongeza;

“Lengo kubwa ni kuonesha kuwa marapa wa Dansi nchini wapo lakini hawapewi kipaumbele. Wao ndiyo waongozaji wa sebene katika bendi zao lakini inajulikana zaidi bendi kuliko wao,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa burudani nzima inatarajiwa kuanza mapema kuanzia saa mbili usiku mpaka majogoo kwa kiingilio cha shilingi 7,000 tu,” alimaliza Mbizo.

SHILAWADU WA CLOUDS TV WANAKULETEA UBUYU MTAANI KWAKO