×

Ndege Ya Jeshi Ya Russia Yaanguka Baharini Sochi

 sochi-1

 Ndege kama hii ya  ya jeshi la Russia aina ya Tupolev Tu-154 iliyoanguka katika bahari ya Black Sea .

NDEGE ya jeshi la Russia aina ya Tupolev Tu-154 ikiwa na watu 92, ikiwemo kwaya ya jeshi, imeanguka katika bahari ya Black Sea karibu na mji wa Sochi, baada ya kuondoka uwanjani.

Wizara ya ulinzi nchini humo  imetangaza kwamba hali inavyoonekana ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyenusurika katika ajali hiyo.

Vyombo vya habari vya eneo hilo, vikinukuu wizara ya ulinzi ya Russia, vilisema ndege hiyo ilikuwa imeondoka katika mji wa kusini mwa Russia wa Adler leo asubuhi na ilikuwa ikielekea Latakia nchini Syria.

sochi-2

Orodha ya abiria na wafanyakazi katika ndege hiyo  iliyotolewa na wizara ilionyesha kwamba kulikuwa na wanakwaya 64 wa kundi maalum  ya jeshi lijulikanalo kama Alexandrov Ensemble pamoja na kiongozi wake Valery Khalilov.

Wanakwaya hao walikuwa wakienda Syria kusherehekea Mwaka Mpya na majeshi ya Russia yaliyoko huko.  Wizara hiyo ilisema pia kwamba miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na daktari mmoja maarufu nchini humo

Mpaka Home; Haya Ndo’ Maisha Halisi ya Darassa, Cheki Anavyopika Msosi Gheto