
Mkali wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa akiunda Kundi la Wakali Kwanza, Q Jay akifanya mahojiano na Global TV Online.

Mahojiano yakiendelea.

Q Jay akiwa na Mfanyakazi wa Global Publishers, Azizi Hashim4 trbf4
MKALI wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa akiunda Kundi la Wakali Kwanza, Q Jay kwa mara ya kwanza tangu arudie Bongo Fleva baada ya kuwa ameokoka, amefungukia projekti yao ya kundi kuwa imeshakamilika na mwezi wa kwanza (Januari) wanarudi rasmi.
Akizungumza na Global TV Online kupitia Kipindi cha Exclusive, Q Jay ambaye kwa sasa anaunda Kundi la Busy Boy akiwa na D Malick alisema kuwa, kwa muda mrefu amepitia maisha magumu yaliyomfanya kupotea katika muziki.
“Nimerudi tena nawaomba mashabiki mnipokee. Nimetoa ngoma ya Nisamehe na Januari nitaachia video yake. Matatizo na stress nilizokuwa nazo ndiyo yalisababisha kutofanya muziki kwa kiwango lakini sasa hivi kila kitu kinaenda sawa.
“Nina projekti na kundi langu la zamani la Wakali Kwanza ambapo tumeshakamilisha kila kitu na MJ na Januari mwakani tutaachia mzigo mzima,” alisema Q Jay.
Q Jay amezungumza stori ya kusikitisha kutokana na kilichomtokea katika maisha yake hadi kushindwa kuimba muziki na kukimbilia jijini Mwanza.
Mahojiano hayo unayapata Global TV pekee kupitia www.globaltvtz.com