ZANZIBAR: Moto wa vijana wa Kimataifa, ambao ndiyo mabingwa wa Tanzania Bara, timu ya Yanga umepelekwa rasmi visiwani Zanzibar kwa kuizaba Jamhuri ya Pemba jumla ya mabao 6-0 katika mchezo wake wa Kwanza wa Kombe la Mapinduzi visiwani humo.
Katika mchezo wa jana, safu ya ushambuliaji ya Yanga ikiongozwa na Donald Ngoma, na Saimon Msuva ilikuwa ni mwiba mkali kwa wapemba hao, kiasi cha kuanza kuruhusu mvua ya mabao katika dakika ya 19 kwa bao la Saimon Msuva, ambaye alifunga pia bao la 4 dakika ya 40.
Donald Ngoma, alipachika bao la 2 dakika 23 na bao la tatu dakika ya 37 kutoka na uzembe wa mabeki wa Jamhuri kushindwa kumdhibiti raia huyu wa Zimbabwe.
Bao la tano lilifungwa na Thaban Kamusoko kwa kichwa akinganisha kros ya Emmanuel Martine kutoka winga ya kushoto katika dakika ya 59 ya mchezo.
Yanga iliyochezesha kikosi chake kamili haikuridhika mabao hayo na kuongeza mashambuliza makali ambapo Juma Mahadhi aliyetokea benchi aliipatia bao la sita kwa mkwaju mkali na kufanya hadi mechi hiyo inamalizika, Yanga wameondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 6-0 na kuongoza kundi hilo la A kwa point 3 na mabao ya kutosha.
Yanga inashika nafasi ya pili katika ligi kuu Bara, wakati Jamhuri pia ikishika nafasi ya pili katika ligi ya kisiwani Pemba.
Mchezaji Greyson Gerald wa Jamhuri amefanikiwa kuibuka mchezaji nyota wa mchezo huo wa le.
Leo ni Jang’ombe Boys dhidi ya URA, huku Simba akikipiga na KVZ.