Malkia wa mtandao mwenye nguvu ya watu wasiopungua milioni mbili na nusu nchini Tanzania, Wema Abraham Sepetu, mwaka 2017 ameuanza tofauti kidogo katika mawasiliano ya data na maisha ya mitandaoni.
Malkia huyo asiyeishiwa matukio, amefuta picha zote katika mtandao wake wa Instagram na katika picha ya mbele ikionekana kivuli tu.
Muonekano wa Account yake kwa sasa Instagram.
Haijafahamika ni kwa nini Wema amefuta picha na video zote katika mtandao huku mitaani upo uvumi wa maneno kwamba huenda ameona mwaka 2017 azaliwe upya katika mtandao kwa kujaribu kuyafuta maovu yake na kuwa mpya ili awe msaada na kiigizo chema kwa jamii.
Wema Sepetu.
Na Salum Milongo/ GPL