×

Waporaji wa Kim Kardashian Wadakwa

kim-kardashianWATU zaidi 15 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kumvamia na kumpora nyota wa vipindi vya televisheni huko Marekani Kim Kardashan.

Mwanadada huyo aliporwa vitu vyenye thamani ya takribani shilingi bilioni 24 huko Paris nchini Ufaransa mwaka jana. Aidha Kim amekuwa akiripotiwa kuvamiwa na kuporwa mara nyingi hii kutokana na kutangaza mali zake mitandaoni. Kim baada ya kuvamiwa na majambazi na kuporwa vitu vya thamani, amesema haweki tena mali zake kwenye mtandao.