Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa FIFA
Ronaldo, 31, amewafunika wapinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwezi Desemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa na timu ya taifa ya Ureno.
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri ametajwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, huku Silvia Neid, meneja wa zamani wa Ujerumani, akishinda kwa upande wa wanawake.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino amkabidhi Cristiano Ronaldo tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora wa Kiume. pic.twitter.com/Gz8h9wmVZa
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Meneja wa @Leicester_News, @DonRanieri ashinda tuzo ya# FIFA ya Kocha Bora wa Mwaka. pic.twitter.com/9swResFXV2
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Silvia Neid kutoka Ujerumani ashinda tuzo ya FIFA ya Mwamuzi Bora wa Kike mwaka 2016. #TheBest pic.twitter.com/nsQQs6XHj2
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Mohd Faiz Subr ameshinda tuzo ya FIFA ya Puskas kufuatia goli alilofunga dhidi ya Pahang katika ligi kuu ya Malaysia 16 Februari 2016. pic.twitter.com/vyPcnQGOvE
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Tuzo ya FIFA ya Mashabiki Bora imekwenda kwa mashabiki wa Borussia Dortmund ya Ujerumani na Liverpool ya Uingereza. pic.twitter.com/xZGjl7Lz1i
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Klabu ya Atletico Nacional ya Colombia yapewa tuzo ya 'FIFA Fair Play
Award' baada ya kutaka Chapecoense wapewe kombe la Copa Sudamericana. pic.twitter.com/yp7cdSZkLd— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Brasileño Falcao raia wa Brazil ashinda tuzo ya FIFA ya 'Outstanding Career.' pic.twitter.com/hMaSFn4QTe
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
Kikosi Bora cha Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) mwaka 2016. Hakuna mchezaji anayecheza ligi kuu ya Uingereza. pic.twitter.com/IKn1zGaORX
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017
#Barcelona hawajahudhuria katika hafla ya utoaji tuzo za 'The Best' wakijiandaa na mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Athletic Bilbao. pic.twitter.com/sVKp4GAV9r
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 9, 2017