



Dk 78, Martin anawatoka Mkude na Muzamiru wanaogongana na yeye anaachia mkwaju mkali hapa. Agyei anaonyesha umakini na kudaka vizuri hapaSUB Dk 77, Simba wanamtoa Luizio nafasi yake inakwenda kwa Pastory Athanas
Dk 76, mpira bado unachezwa sana katikati ya uwanja na Yanga wanaonekana kuanza kukontrooo mpira zaidi ya Simba

Dk 68, Yanga wanachonga kona safi, kichwa cha Mwinyi mpira unakwenda nje
Dk 61 sasa, mpira bado unachezwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 55, kosa hapa Dante anachichanganya Simba wanaingia hatariiiiiii Dante anaokoaDk 54, kona ya Kichuya, hatari tena, Dida anaokoa hapa
Dk 53, Kichuya anaingia vizuri hapa, hatariiii lakini Dante anamuwahi na kutoa nje, kona

Dk 53, Juma Abdul anacheza faulo hapa lakini mwamuzi anamsamehe, akimuonya kwa maneno. Kumbuka kadi ya njanoDk 52 kona nyingine inachongwa na Kotei lakini Yanga wako makini wanaokoa
Dk 51, Simba wanafanya shambulizi kali hapa, krosi ya Kichuya Yondani anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya, Dida anaokoa tena na kuwa kona tena

Dk 47 krosi nzuri ya Mwinyi lakini Mwanjale anauwahi, kona. Inachongwa na Niyonzima , wanaokoa
Dk 46, Yanga wanacheza vizuri, lakini Tambwe anashindwa kupiga krosi kutokana na kasi ya mpira
Dk 45, Kipindi cha pili kimeanza na inaonekana suala la hofu kwa wachezaji bado limejaa
MAPUMZIKOKADI Dk 45, Mwamuzi anatoa kadi ya njano kwa Abdi Banda kumuangusha Kaseke, kadi ya njano kwa Juma Abdul
Dk 43, hatariiiii, Msuva anapoteza mpira, Mo Ibrahim anaachia fataki, Dida anaugusa na kutgonga mwamba, unamkuta Luizio anaachia shuti, goal kick
Dk 40, Banda anaachia fataki lakini mpira unawagonga mabeki wa Yanga, wanaokoa

KADI Dk 39, Mwingi analambwa kadi ya njano kwa kumrukia Mo Ibra
Dk 37, Msuva anamtoka Zimbwe kwa mara ya kwanza, anaingia vizuri na kujaribu kupiga lakini mpira anaukosa na Bukungu anauokoa kabla haujavuka lango
Dk 28, Yanga inapata kona baada ya Simba kuukoa mpira wa faulo wa Mwinyi, inachongwa lakini kipa anafanyiwa madhambi
Dk 21 sasa, mambo bado, mashambulizi si mengi. Simba hasa Banda wanapaswa kuwa makini na kupunguza mipira isiyokuwa na maana karinu lango lao
Dk 18, mkwaju mkali wa Mwinyi wa faulo, unatoka kidogo nje ya lango la Simba
Dk 16, Mo Ibrahim, anaachia shuti kali katikati ya msimu wa mabeki wa Yanga, Dida anadaka vizuri kabisa
Dk 15, Yanga wanapoteza nafasi, Msuva anapiga shuti lakini Banda anakaa chini na kuzuia. Ilikuwa nafasi nzuri kwa YangaDk 10 sasa, kila upande unaonekana kuwa makini sana kwa sababu hakuna mashambulizi mengi kwenye milango
Dk 8, Banda anapiga kichwa mpira unamkuta Niyonzima, anaingia vizuri na kuachia shuti kali hapa, Agyei anadaka vizuri kabisa
Dk 7, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja ingawa Simba ndiyo wanaonekana kutawala zaidi katikati ya uwanja