×

Costa: Nachukia Soka la Uingereza

costa_3082271bLONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Chel­sea, Diego Costa, ame­onyesha kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo wakati wowote, aliposema kuwa analichukia soka la England.

Kocha wa timu hiyo Antonio Conte, alimuondoa mshambuliaji huyo kwenye kikosi chake kilicho­vaana na Leicester City wikiendi iliyopita kwa kile kilichodaiwa kuwa alikorofishana na mmoja kati ya makocha wa timu hiyo.

Costa, 28, yupo kwenye mkata­ba na timu hiyo hadi mwaka 2019 na Chelsea waligoma kumuuza kwenye usajili wa majira ya joto yaliyopita, lakini sasa inaonekana kuwa anaweza kuondoka.

Taarifa zinasema kuwa Conte atakuwa na kikao na mchezaji huyo kesho kujadili kuhusu sakata hilo.

“Diego alifanya mazoezi Ju­manne na kusikia maumivu kwenye nyama za miguu, haku­fanya mazoezi tena na kwa sababu hiyo akakosekana kwenye mchezo uliopita,” alisema kocha huyo.

Gazeti la SunSport limeripoti kuwa linajua mchezaji huyo aliko­rofishana na kocha wa viungo mazoezini na wakala wake ame­kuwa akipambana sasa kuhakiki­sha kuwa anamtafutia timu nchini China.

Inaelezwa kuwa aliwaambia wenzake kuwa atafanya kila li­nalowezekana ili aondoke kwenye timu hiyo kwa kuwa analichukia soka la England pamoja na Chama cha Soka England (FA).

Chanzo kutoka nchini China kimesema: “Costa ni chaguo la kwanza hapa, tunajua kuwa ana­taka kuja kucheza huku.”