SENEGAL: BAADADA ya vuguvugu la kisiasa lililotokana na utata wa nani mshindi halali kwenye uchaguzi wa Gambia wa mwezi jana, hatimaye leo usiku, Adama Barrow aliyetajwa na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo.
Barrow amekula kiapo hicho akiwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal na mataifa yote kumtambua kuwa yeye ndiye rais halali wa nchi hiyo kuanza sasa huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi zao.
Ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Lakini aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh amekataa kujizulu na muda wake wa kuhudumu umeongezwa na bunge a nchi hiyo jana hadi miezi mitatu ijayo.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameshindwa kumsihi Jammeh kuondoka mamlakani kwa amani na kumtishia kumuondoa kwa nguvu. Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kwenye hafla hizo ni balozi wa Rwanda nchini Senegal.
Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi huo wa Disemba 1, 2016, kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo lakini anataka matokeo ya uchaguzi huo yafutwe akidai makosa mengi katika uchaguzi huo.
Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow.
Kiapo cha Barrow
”Mimi Adama Barrow naapa kwamba nitatekeleza wajibu wangu katika afisi ya urais wa taifa la Gambia kwamba nitahifadhi na kutetea katiba” .
Na katika hotuba yake ya kuapishwa, amewaagiza wanachama wote wa jeshi la gambia kusalia katika kambi zao. ”Wale watakaopatikana wakibeba silaha watachukuliwa kuwa waasi”, alionya.
Barabara za Gambia.
Wasifu wa rais mpya wa Gambia Adama Barrow
-Adama Barrow alizaliwa mwaka 1965 katika kijiji kimoja karibu na mji wa kibiashara wa Basse Mashariki mwa Gambia.
– Alihamia mjini London miaka ya 2000 ambapo anaripotiwa alifanya kazi kama mlinzi kwenye duka moja, Kaskazini mwa London, akiendelea pia na masomo yake.
– Alirejea nchini Gambia mwaka 2006 ambapo alianzisha kampuni yake ya kuwekeza.
-Barrow mwenye umri wa miaka 51 aliteuliwa kuongoza muungano wa vyama saba vya upinzani kumpinga Rais Yahya Jammeh.
-Amekosoa kutokuwepo kwa miula miwili kwa urais na pia kulaani kufungwa kwa wanasiasa wa upinzani.
-Anaunga mkono uhuru wa mahakama, wa vyombo vya habari na wa vyama vya umma.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh aliyemaliza muda wake.
Wanajeshi wanaomtii Jammeh kukabiliana na uvamizi wowote
Rais wa Gambia Yahya Jammeh mpaka jioni alikuwa katika makao yake rasmi kwenye ikulu ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP lililomnukuu afisa mmoja nchini humo ikiwa atakamatwa na kikosi cha kanda basi atakuwa katika ikulu na wengi wa wanajeshi wanaomtii Jammeh watapinga hilo.
Vikosi vya kanda vinatarajiwa kuchukua hatua. huku Senegal imetuma mamia ya wanajeshi kwenye mpaka wake na Gambia huku Nigeria ikituma ndege za kivita na helikopta mjini Dakar, na pia imepeleka meli ya kivita eneo hilo.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa baadhi ya wanajeshi wa kanda tayari wameingia nchini Gambia.
This is a victory of the Gambian nation. Our national flag will fly high among those of the most democratic nations of the world. #Gambia pic.twitter.com/QRGZg1gzbs
— Adama Barrow (@adama_barrow) January 19, 2017
It is time. #NewGambia pic.twitter.com/VNXY1h3Ds5
— Adama Barrow (@adama_barrow) January 19, 2017
You can change your politics, but never can you change your favourite football team! Thank you — @Arsenal! #Gambia #Arsenal pic.twitter.com/Pr1yFq58AK
— Adama Barrow (@adama_barrow) January 7, 2017