×

Droo ya Kwanza Kutingisha Feb 8, Zawadi Kibao Kutolewa

shuinda-nyumba-9

Mr. Uwazi akiwaelekeza wasomaji Gazeti la Uwazi namna ya kushiriki Shinda Nyumba, juzi Jumanne maeneo ya Goba jijini Dar.

BAHATI Nasibu ya Shinda Nyumba awamu ya pili imeanza kunoga ambapo  droo ya kwanza inatarajiwa kutimua vumbi Februari 8, 2017 jijini Dar ambapo washindi watajinyakulia zawadi kibao, zikiwemo pikipiki, TV, simu za kisasa na vyombo vya ndani.Nyumba (7)

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho,  droo hiyo ya kwanza, itawapata washindi wanne ambao watajishindia pikipiki, televisheni, simu ya kisasa (SmartPhone) na vyombo vya ndani.

shinda-nyumba-9

Wasomaji wakichangamkia gazeti la Uwazi.

“Wasomaji wahakikishe wanajipatia kuponi za kutosha tayari kwa droo yetu ndogo ya kwanza ambayo itafanyika hiyo Februari 8, mwaka huu.

shinda-nyumba-arusha-7 Wakazi wa Arusha wakifurahia uzinduzi wa Shinda Nyumba.

Kama wanavyoona, katika siku yake ya kwanza tu, tunatoa zawadi hizi ambazo zinatosha kabisa kubadilisha maisha ya mshiriki, huu si wakati wa kuupoteza.

shinda-nyumba-28

“Sehemu hasa itakapofanyika droo hii tutaitangaza ndani ya muda mfupi ujao, lakini kwa vyovyote itakuwa ni hapa Dar es Salaam, utaratibu wetu wa kutuma kuponi ni uleule, baada ya kununua gazeti letu lolote kati ya Championi, Risasi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, kata kuponi kisha jaza kwa kadiri ilivyoelekezwa, halafu peleka kwa wakala yeyote aliye jirani na wewe, maana mawakala wetu wapo nchi nzima, au kwa wale wa Dar es Salaam, wanaweza kuleta katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar,” alisema.

shinda-nyumba-23Wakati hayo yakitangazwa, miji ya Mbeya, Arusha na Mwanza, kwa nyakati tofauti wiki iliyopita, nayo ilifanya uzinduzi wa promosheni ya shindano hilo, huku wasomaji wakazi wa maeneo hayo, wakisisitiza kuwa hii ni zamu yao ya kuibuka washindi baada ya Nelly Mwangosi wa Iringa kupata nyumba ya mamilioni, mwaka jana.

“Kabla ya kupatikana kwa mshindi, tulijua haya ni mambo ya mipango tu, si unajua tena maana haikuwahi kutokea kampuni ya magazeti ikatoa zawadi kubwa kiasi kile, kwa hiyo wengine tukaona shinda-nyumba-18hebu acha tuone, lakini baada ya mshindi kupatikana, tumegundua hii kitu ilikuwa ni kweli,” alisema Joshua Laiser wa Kijenge mkoani Arusha.

Laiser alisema mwaka huu utakuwa ni msimu wa watu wa Kanda ya Kaskazini na bila shaka, yeye ndiye atakuwa mshindi kwa niaba yao.

shinda-nyummba-mbalizi-8… Wakijaza kuponi.

“Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa magazeti ya Global Publishers ila nilikuwa sitilii maanani mashindano yaliyokuwa yakiendeshwa kutokana na kutoamini kama mshindi anapatikana bila kupangwa, ila baada ya kuona mshindi wa awamu ya kwanza kapatikana kutoka Iringa, tena ni mwanamke mjasiriamali, nikashawishika sana na sasa tutakula sahani moja mpaka kieleweke,” alisema Laiser.

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam