×

Hatimaye Rais Barrow Awasili Gambia

barrow1

Maelfu ya wananchi wa Gambia wamefurika katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul kumlaki Rais wao, Adama Barrow wakati akiwasili nchini mwake kuiongoza nchi hiyo baada ya kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya Jammeh.
Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi uliompa ushindi Barrow.
barrowBarrow ameamua kurudi nchini humo mapema baada ya Wanadiplomasia kumtaka arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi.
Kutokana na taarifa zinazoeleza kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini, maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia ili kuimarisha ulinzi kwa Rais Barrow.

gambia-barrow

Barrow atakaa katika makazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika Ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam