
MPIRA UMEKWISHA; Matokeo, Azam FC 1- 0 Simba SC.
Dk 90+4; Simba wanashambulia kaunta atack, wanapata kona hapa. Tayari kona imepigwa lakini haijazaa matunda.
Dk 90+ 1; Manula yko chini ameanguka baada ya kuchezewa madhambi.
Dk 90; DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89; Mavugo anapiga kichwa mujarabu lakini Manula anapangua, inakuwa kona kuelekea Azma.
Dk 83; Azam FC wanafanya mabadiliko, Abdallah Kheri anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya John Bocco.
Dk 82; Manula anapigwa kadi ya njano na mwamuzi Onoka baada ya kupoteza muda kwa kukaa na mpira.
Dk 80, Bocco yuko chini hapa akiwa ameshika paja lake
Dk 78, Zimbwe anapokea pasi na Mavugo, anawatambuka mabeki wa Azam na kuachia mkwaju lakini hakulenga lango
SUB Dk 76, Simba wanamuingiza Mudathir kuchukua nafasi ya Kingue ambaye ameumia
Dk 73, Stephan KIngue wa Azam yuko chini anatibiwa hapa, anatolewa nje na
Dk 70; GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOAl, Azam FC wanapata bao kupitia kwa John Boko dakika ya 70 baada ya kufanya kaunta attack. Simba bado hawajapata bao.
Dk 68, Simba wanafanya shambulizi tena, krosi nzuri, Ajib yeye na lango anashindwa kupiga kichwa kulenga, gooal kick
Dk 68; Mavugo langoni mwa Simba anapiga kichwa anakosa bao la wazi kabisaaa.
Dk 66, Kichuya anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Manula anaudaka vizuri hapa

SUB Dk 64; Simba wanafanya mabadiliko, Laudit Mavugo amvugo anaingia kuchukua nafasi ya Juma Luzio.
SUB Dk 62; Azam wanafanya mabadadiliko, Singano anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Yahya Mohamed.

Dk 60; John Boko ananda anaondoka lakini anapigwa tackling na mpira unatoka nje.
Dk 58; Simba wanafanya mabadiliko, Ibrahim Ajib anaingia kuchukua nafasi ya Bukungu.
Dk 54, mechi imesimama kwa dakika moja baada ya Bocco kumtwanga teke Boukungu wakati akiachia shuti kwa lengo la kufunga. Inaonekana ilikuwa ni bahati mbaya.

Dk 51, Mpira unaonekana kuchangamka sasa, timu zinaanza kufunguka na kucheza mipira mirefu na kufanya mashambulizi
Dk 47; Simba wanakosa bao hapa langoni mwa Azam.
SUB Dk 46, Simba inafanya mabadiliko ya kwanza, Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Jamal Simba Mnyate
Dk 45; Tayari mpira umeanza kipingdi cha pili.

MAPUMZIKO
Dk 45+1; Timu zote zimepoa sana leo, zinaviziana.
Dk 45; Zinaongezwa dakika 2.
Dk 44, Manula anafanya kazi nzuri kwa kutokea na kuudaka mpira wa krosi kabla haujamfikia Athanas
KADI Dk 43, Singano naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo dhidi ya Banda na alipoitwa na refa akamfokea.

Dk 41; Athanas anamgeuza Yakubu ndani ya boksi anaachia fataki lakini mpira unapaa sentimita chache kutoka kwenye mtambaa panya na kutoka nje kuwa goal kick.
Dk 39, Simba wanaingia eneo la hatari la Azam, Muzamiru anaachia shuti lakini linakuwa nyanya hapa kwa Manula
Dk 33; Erasto Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Pastory Athanas, hii ni kadi ya kwanza ya njano ya mchezo huu.
Dk 32; Singano anaondoka lakini, anafanyiwa madhambi langoni mwa Simba, Tayari azam wameshaanza hapa na mpira unaendelea.

Dk 30; Mpira umepoa sana, timu zote zinashambuliwa kwa kuviziana.
Dk 26; Singano anaunawa mpira na inapigwa faulo kuelekea Azam.
Dk 24; Singano anaondoka, anaingia hapa, anampa Gabriel Michael anaachia krosi kali lakini Azam wanapotea langoni mwa Simba, wanashindwa kumalizia.
Dk 23, Yakubu anautoa mpira nje na kuwa kona ya kwanza ya mchezo ambao wanaipata Simba. Inachongwa hapa Azam FC wanaokoa
Dk 20; Simba wanajaribu kuingia langoni mwa Azam, Manura anakamata mpira kwa mara ya kwanza.
Dk 19; Boko tena anataka kuondoka, lakini Mwanjali anamdhibiti vilivyo.
Dk 15, Mahundi anapoteza nafasi nzuri ya kwanza baada ya kuupata mpira kwenye boksi la Simba mabeki wakiwa wamezubaa, anapiga shuti la chini, mpira unampita Agyei na kuwa goal kick

Dk 14; Joseph Mahundi anakoswa bao tena, alizan ameotea akajistukia, amepiga, Agyei anakuwa makini na kuudaka mpira huo.
Dk 12; John Boko anakosa bao hapa langoni mwa Simba, alitaka kuwamaliza mapema mapema lakini kipa akawahi kuubabatiza ukaenda pembeni.
Dk 9, Bukungu anaachia shuti kali lakini linatoka nje. Kinachoonekana timu hizi kila mmoja imejaza watu wengi zaidi nyuma, hivyo kufanya kusiwe na ladha ya juu ya ushambulizi

Dk 6 sasa, hakuna shambulizi hata moja kali. Zimbwe wa Simba anatolewa nje baada ya kugongana na Mhundi, anapatiwa matibabu
DK 4: John Boko anataka kuwatoka mabeki wa Simba lakini anakuwa offside, upande wa pili Shabalala yuko chino haijulikani amekutwa na nini.
Dk 1; Tayari mchecho umekwisha anza, Joseph Mahundi wa azam anaachia shuti lakini kipaAgyei anaunyaka.
Timu zimeingia uwanjani tayari
PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA/GPL