×

Kabila la wala watu-4: Aliyemuua na kumla mtoto wa makamu wa Rais wa Marekani apatikana, ajieleza

wala-nyamaKIJANA Michael Rockefeller aliliwa na watu hao wa visiwa vya Papua New Guinea. Imekuja kugundulika baada ya miaka mingi kupita kuwa aliliwa kwani kijana huyo ambaye baba yake aliwahi kuwa gavana wa Jiji la New York na baadaye Makamu wa Rais wa Marekani, Nelson Rockeeller mwaka 1961, alikwenda katika visiwa hivyo kwa nia ya kufanya utafiti juu ya watu hao. Enzi hizo,kulikuwa na watu ambao walikuwa hawaamini kwamba kuna binadamu anaweza kumfanya mtu kitoweo kwa kumuua na

kumkatakata vipande kisha nyama yake kuibanika na kuila. Michael alikwenda katika visiwa hivyo kwa nia hiyo ya kuhakikisha ukweli wa habari hiyo. Hata hivyo, hakurudi japokuwa katika picha zake ambazo alipiga na baadaye ‘negativu’

zake kupatikana na kuchapishwa katika magazeti, zilionesha kuwa alipokelewa vizuri na watu hao. Kuna baadhi ya picha alionekana akiwa na wala nyama za watu hao,

wakimshangilia wakiwa na watoto wao na wanawake huku yeye Michael akiwa katikati yao akiwapiga picha na wote wakiwa na tabasamu. Wenyeji hao wala watu ni wa ukoo wa Asmat huko Papua New Guinea, lakini ajabu ni kwamba baadaye alitoweka na hakujulikana yupo wapi. Ilimlazimu Nelson, baba yake mzazi

kufunga safari na kwenda katika nchi hiyo kwa lengo la kumtafuta mwanaye.      Hata hivyo, hakuweza kumpata kwani alirudi mikono mitupu na baadaye ukaanzishwa utafiti maalum ili kubaini kama yu hai au

ameshaliwa

na watu hao. Utafiti huo uliofanywa na Netflix, ulipewa jina la The Search For Michael Rockefeller ambapo mwaka 2014 ilithibitika kuwa  Michael, mtoto wa mwisho wa Makamu wa Rais wa Marekani, Nelson Rockefeller, aliliwa na watu hao. Watafiti hao walifanikiwa kumpata  mtu aliyemuua kwa

kumchinja (angalia pichani, mwenye ndevu) na alipohojiwa alikiri kufanya unyama huo na kumla nyama pamoja na wenzake. Alisema mara baada ya kumuua kama ilivyo desturi yao, Michael alikatwakatwa na nyama yake kubanikwa kisha kuliwa na watu maalum ambao huwa wanajipakapaka rangi nyeupe na nyeusi miili yao kwa kujifanya kama vile wachawi.

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina moja la Ajam ambaye picha zake zipo katika mitandao, haikusemwa kama alifanywa chochote na serikali ya Papua New Guinea baada ya kukiri kuua na kula nyama za watu na washirika wake. Yeye alipoulizwa alimsukumia ukatili huo kiongozi wake

ambaye ni chifu wa ukoo wa Asmat katika visiwa hivyo. Alisema alifanya hivyo kwa amri ya chifu wao ambaye pia alipatikana na watafiti hao (pichani juu mwenye manyoya kichwani). Mzee huyo alikuwa wazi kwa kusema kwamba alikuwa na kawaida ya kula nyama za Wazungu kwa sababu maalum.

ITAENDELEA WIKI IJAYO.