×

Davina Aruka Kimanga Skendo ya Usagaji

HALIMA Yahya ‘Davina’

Na Gladness Mallya: RISASI MCHANGANYIKO

HALIMA Yahya ‘Davina’ mmoja wa waigizaji nyota nchini, ambaye amekuwa akitajwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameruka kimanga na kusema kamwe hajawahi kuwa msagaji na wala hajui ‘mchezo’ huo unachezwaje.

HALIMA Yahya ‘Davina’

Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kilisema, Davina amekuwa akifanya mchezo huo na msanii mwenzake (jina limehifadhiwa) kwa sasa na kuwa wamekuwa wakionyeshana vitendo vya kimahaba hadharani pasipo kujali chochote.

Za Motomoto News ilimtafuta Davina ambaye alifunguka hivi; “Jamani (anamtaja msanii huyo) ni rafiki yangu wa kawaida tu, mimi nina watoto na hizo tabia za usagaji sina kabisa wala sijui hata huwa wanaf  anyaje naona watu wanataka tu kuniharibia sifa yangu kwa jamii.”