
Alfred Shauri akizungumza jambo wakati alipotembelea ofisi za Global Publishers leo.
Dar es Salaam: KIJANA Alfred Shauri (17), aliyeongoza kwenye matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2016, yaliyotangazwa jana na Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde, leo ametembelea ofisi za Global Publishers, wachapishaji wa gazeti hili na mengine ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda na Championi ambapo alizungumza mambo mbalimbali, ikiwemo siri yake ya ushindi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo (wa pili kushoto) akizungmza na Alfred baada ya kutembelea ofisi hizo.
Akizungumza kwa kujiamini, Alfred alisema katika maisha yake hajawahi kufeli mtihani lakini pia hajawahi kufaulu kwa kiwango anachokitaka.
Alfred ambaye amehitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza ya jijini hapa, alisema alizipokea taarifa za kuongoza mtihani huo kwa mshtuko mkubwa kwani licha ya uwezo wake mkubwa, hakutegemea atakuwa wa kwanza kitaifa.

“Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi huu nilioupata, baada ya kupokea matokeo hayo jana, nilikuwa ‘surprised’ sana.
“Nilitegemea kufaulu vizuri kulingana na maandalizi niliyokuwa nimefanya, maandalizi yalianza mapema tangu nikiwa kidato cha kwanza, kwani mtihani wa kwanza tu nilipata wastani wa 87 na bado nikawa wa 21 darasani hivyo sikukata tamaa, nilikaza na leo namshukuru Mungu,” alisema Alfred huku akicheka.
Shigongo akimuelekeza jambo Alfred
Kuhusu mbinu alizotumia mpaka kupata nafasi aliyoipata kwenye matokeo hayo, Alfred alisema ni kujitambua, kujituma na kuendelea kujiboresha kila mara kwa kila jambo analofanya hasa darasani.
Katika hali ya kushangaza, Alfred alisema alikuwa na utundu wa chinichini shuleni, huku upole wa sura yake ukiwafanya hata walimu wamtetee anapofanya makosa.
Alfred aliambatana na mwalimu wake wa masomo ya sayansi, Mwalimu Senyagwa (kulia)
“Nilikuwa msumbufu sana, nakumbuka nimewatesa sana wanafunzi wenzangu maana nilikuwa na kundi langu, sema ilikuwa wakienda kunishtaki kwa walimu, wananitetea kwa sababu ya upole wangu, kwa kweli naomba sana Mungu anisamehe kwa hili,” alisema.
ovuti yako namba moja nchini, Global Publishers imekuwekea matokeo yote Kitaifa, usisumbuke msomaji wetu!
BOFYA HAPA KUYAONA===> MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016
BOFYA HAPA KUYAONA===> MATOKEO MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2016