
Ramsey Nouah
MMOJA kati ya wakongwe walioiweka filamu Nollywood katika ramani ya dunia, Ramsey Nouah kwa mara ya kwanza amemfungukia mkewe, Emelia Philips ambaye ameishi naye kwa zaidi ya miaka 15.
Akijibu moja ya swali aliloulizwa katika mahojiano na Gazeti la Premium Times kw amba amewezaje kuishi na Emelia kwa zaidi ya miaka 15 bila kuwa na misukosuko, Ramsey anayetikisa na Muvi ya 30 Days in Atlanta na 76’ alisema:
“Mke wangu si wa kizamani. Anajua vitu vingi kwenye filamu ambavyo wasichana wengi hawajui na ndiyo maana nasema, muigizaji wa kike ama wa kiume anatakiwa kuwa na mtu sahihi wa kuishi naye.

Ramsey na mkewe.
“Mke wangu ananichukulia zaidi ya rafiki. Anajua siwezi kumpoteza kisa nimempata mwanamke mwingine, haiwezekani!”