×

Kuwa wa Kwanza Kuziona Picha Mtoto Nillan Hapa

Diamond akiwa amembeba mwanaye Nillan, wengine ni mwanaye mwingine Tiffah na Zari.

Diamond akiwa na mwanaye Nillan.

Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Zari, Diamond na Nillan, Tiffa, Zari na mama Diamond.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Diamond Platnumz, leo amemfanyia sherehe ya arobaini mwanaye Nillan ambapo kwa mara ya kwanza, mtoto huyo ameoneshwa sura hadharani katika sherehe ya aina yake, iliyofanyika nyumbani kwao, Madale jijini Dar es Salaam.

Nillan, mtoto wa kiume, ni wa pili kwa Diamond na Zari, akitanguliwa na Tiffa ingawa upande wa Zari, anao watoto wengine wanne, aliozaa na mwanaume wake wa awali, Ivan Ssemwanga, raia wa Uganda.

Nillan alizaliwa nchini Afrika Kusini, yalipo makazi ya mwanamama Zari na tangu kuzaliwa kwake, hakuwahi kuoneshwa sura hadharani hata siku moja mpaka siku ya arobaini yake.

PICHA ZOTE NA BEKKA ISSA | GLOBAL PUBLISHERS

 

Save