×

Pichaz: Kinachojiri Madale Kwenye 40 ya Mdogo wa Tiffah Diamond

Mandhari ya nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar yalivyo leo.

Wageni wakiwa wamepozi kabla ya shughuli kuanza.

Baadhi ya mastaa wa filamu wakipiga picha ya pamoja na mama Diamond, Sandra na Esma wakati wa maandalizi ya shughuli hiyo.

Palivyonoga.

Msanii wa filamu na muziki nchini, Isabella Mpanda akipozi wakati akisubiria kuanza kwa shughuli hiyo.

Isabella na Mama Rolaa wakipozi.

WASANII kibao pamoja na watu maarufu wamejitokeza kwa wingi kwenye hafla ya 40 ya mtoto wa pili wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Nillan Nasibu inayoendelea kufanyika nyumbani kwa staa huyo, Madale jijini Dar es Salaam.

Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha mandhari ya nyumbani kwa Diamond na namna palivyopambwa kabla ya shughuli hiyo kuanza rasmi.