×

Yusuf Manji Apelekwa Hospitali na Ambulance

DAR ES SALAM: Mfanyabiashara Yusuf Manji ametolewa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi muda mfupi uliopita na kupandishwa kwenye gari la wagonjwa ambalo lilipita Barabara ya Sokoine kuelekea Posta Mpya.

Kwa mujibu wa chanzo cha tukio hilo,l Manji akipanda gari hilo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lakini hawakufahamu mara moja alikoelekea.

Manji alikuwa amevaa fulana, suruali na viatu vya wazi vyote vya rangi nyeusi.

Gari la wagonjwa lililombeba Yusuf Manji na gari lake binafsi yakiwa katika viunga vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Save