
Moja kati ya matukio yanayotrend kwa upande wa burudani ni pamoja na tuzo za Grammy Awards za mwaka 2017.
Licha ya mastaa wengi kutajwa kuwania tuzo hizo kwenye vipengele tofauti, kwa upande wa Africa macho yote yalikuwa kwa Wizkid ambaye kwa mara ya kwanza alipata fursa ya kutajwa kuwa miongoni mwa wa wasanii watakowania tuzo hizo na rapper Drake kutokana mchango alioutoa kwenye utayarishaji wa album ya ’VIEWS’ ya rapper huyo.

‘One Dance’ ulikuwa miongoni mwa nyimbo zilizokuwa zinawania tuzo ya Grammy usiku wa jana kwenye kipengele cha Best Song of the Year lakini wawili hao (Wizkid na Drake) hawakufanikiwa kubeba tuzo hiyo badala yake waliipoteza kwa Adele na wimbo wa ‘Hello’.
Ushindi wa tuzo hii kwa Wizkid ungeweka rekodi ya kipekee barani Africa kwani wimbo huo wa One Dance pia ni wimbo uliyoandikwa kwa ushirikiano wa Wizkid mwenyewe na ni moja ya nyimbo zilizotrend kwenye playlist kubwa za muziki duniani ikiwemo Billboard 100 Music Chart ya Marekani, na pia ni wimbo uliyosikilizwa zaidi ya mara billion 1 kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza nyimbo; Spotify.