×

Bale Arejea Mzigoni

Gareth Bale

GARETH Bale ameipa klabu yake pamoja na taifa lake matumaini kufuatia kurejea uwanjani kufanya mazoezi. Bale hajacheza tangu Novemba, mwaka jana kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, lakini Real Madrid ilitupia picha na maelezo kwenye Twitter ikimuonyesha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 akifanya mazoezi makao makuu ya klabu hiyo, juzi Jumapili. ameipa klabu yake pamoja na taifa lake matumaini kufuatia kurejea uwanjani kufanya mazoezi.

Bale hajacheza tangu Novemba, mwaka jana kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, lakini Real Madrid ilitupia picha na maelezo kwenye Twitter ikimuonyesha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 akifanya mazoezi makao makuu ya klabu hiyo, juzi Jumapili.

Habari za kurejea kwa Bale, pia zitamfurahisha kocha wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman kuelekea mchezo wa mwezi ujao wa kusaka nafasi ya kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Ireland jijini Dublin.

Wales wanashika nafasi ya tatu katika Kundi D, wakiwa pointi nne nyuma ya Ireland ambao wanaongoza kundi w a k i w a wameshinda mechi tatu pamoja na sare moja katika michezo yao minne. Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, alisema Ijumaa iliyopita kuwa anatumaini Bale atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Napoli Machi 7.