×

VIDE:O: Shilawadu Kuja na Project ya Viatu

WAANDAAJI wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV, Soud Brown na Qwissa wameanika mikakati wanaotarajia kuifanya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kutengeneza na viatu vitakavyokuwa na nembo yao.

Wakifanya Exclusive Interview na Global TV Online wakati wa hafla ya Irene Uwoya Valentines’ Special Night iliyofanyika kwenye Klabu ya Next Dooer Masaki Dar usiku wa kuamkia jana, baada ya kupewa fursa ya kuhojiana wao kwa wao mmoja wa waandaji hao, Qwissa alisema haya.

“Kwa sasa tumeuza piece zadi ya 6000 za ‘ubuyu’, licha ya mwanzo soko kuwa la kusuasua, lakini wiki kama mbili zilizopita order zimeongezeka, hasa siku za Ijumaa na Jumamosi ambapo kipindi kinakuwa kinauka, tunapokea simu nyingi sana za mawakala wakitaka mzigo. Alisema Qwissa.

Kuhusu Next Project vipi?

“Akizungumza kuhusu project ijayo, Qwissa alisema kuwa kwa sasa Shilawadu wanajiandaa kuja na viatu ambavyo vitakuwa na nembo yao na wataviuza mtaani.

“Nachoweza kusema tu ni kwamba, mashabiki wakae tayari, tunasubili project ya Ubuyu ‘’ (iwe imara) mua wowote tunakuja na project ya viatu ambapo tunaamini itatufikisha mbali na kutengeneza kampuni kubwa hapa Bongo.” Alisema Qwissa.

WATAZAME SHILAWADU WAKIZUNGUMZA NA GLOBAL TV

Save