×

Wito: Mamlaka na Taasisi Ziwatumie Wahitimu wa Chuo cha Maji

Mkuu wa Chuo cha Maji cha Dar es Salaam (Water Institute), Dk. Shija Kazumba, akizungumza na wanahabari. Kulia kwake ni Ofisa Habari Mwandamizi wa chuo hicho, George Karumuna .

MKUU wa Chuo cha Maji (Water Institute) kilichoko jijini Dar es Salaam, Shija Kazumba,  ameziomba mamlaka za serikali na taasisi kutumia au kuwaajiri wataalam wa maji wanaomaliza masomo yao kutoka chuo hicho katika shughuli nzima za miundombinu ya maji hadi katika uhifadhi bora wa maji.  

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Hayo ameyasema leo alipozungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, alipofafanua kwamba chuo chake hadi sasa kina wanafunzi 1,849  kati yao wanawake wakiwa 489 hivyo akaomba taasisi na mamlaka mbalimbali kuwatumia wataalam wanaotoka katika chuo hicho kwani tayari wanakuwa wamepata elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya maji kwa jumla.

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia matukio katika mkutano huo.

Alisisitiza kwamba wahitimu wa chuo hicho wote ni bora akimaanisha wanaume na wanawake  ambapo wanaweza kufanya kazi zote zinazohusiana na miundombinu ya maji kikamilifu.

Na Denis Mtima/GPL