
KAMPUNI ya Pama Group Limited, imepinga vikali taarifa ambazo zimeandikwa kwenye vyombo vya habari kuwa ni moja ya kampuni ambazo zinataka kuishitaki serekali kutokana na kusitishwa kwa uzalishali wa pombe za viroba kitu ambacho wamekikana walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Spice iliyopo Mnazi mmoja jijini Dar.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Philipo Magori, alisema kuwa kampuni hiyo haijawahi kufikiria kufanya hivyo hata mara moja na wanashangazwa na mwanasheria ambaye alizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo.
