HIT maker wa ngoma ya Maumivu ‘Khadija Nito’ amejikuta akilia kwa uchungu na kudondosha chozi wakati GLOBAL TV ONLINE ikimfanyia Exclusive Interview. Chanzo cha Khadija kudondoka chozi ni baada ya kuulizwa swali kuhusu mahusiano yake na wazazi wake baada ya kuolewa na Mkiristu ilihali yeye ni Muislam.
“Kiukweli mimi nawapenda sana wazazi wangu, japo kuna watu wamekuwa wakimpelekea mama maneno ili anichukie lakini mimi nasmea ninamheshimu na ataendeea kuwa mzazi wangu tu.
“Naumia sana kukoswa amani ndani ya moto wangu… (alidondosha chozi) na kukakisha interview kwa muda.
Kuhusu uhusiano na mumewe na jinsi anavyosapoti kazi zake, Khadija amesema mumewe anamsapoti kwa asilimia zote na anapenda aendelee kufanya kazi za muziki kwa nguvu zote.
Nisikumalizie uhondo… itazame hii video umsikilize Khadija anavyoteswa na baraka za wazazi kuhusu ndoa yake.