
Wakati jeshi la polisi likiwa bado linaendelea na uchunguzi wake juu ya msanii wa Bongo Fleva Vanessa Mdee, msanii wa hip hop Nay wa Mitego amejitokeza kumpatia pole mwimbaji huyo amabaye bado anashikiliwa na jeshi la polisi.
Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii waliotajwa kwenye orodha ya awamu ya pili na mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda ambaye juzi msanii huyo alijisalimisha kituoni hapo kama alivyotakiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kuhusishwa na madawa ya kulevya.
“Ndio tunamshikilia msanii Vanessa Mdee, tunaendelea na uchunguzi wetu na tukikamilisha uchunguzi wetu na ikathibitika kama ana kosa la kujibu basi tutamfikisha mahakamani,” – alisema Kamishna Sirro kwenye press conference na waandishi wa habari siku ya Ijumaa Machi 10.

Msanii wa Hip Hop Nay wa mitego amejitokeza na kusema kuwa ameguswa na hali iliyomkuta muimbaji huyo wa #CashMadame, na kupitia Instagram page yake Nay alipost picha ya Vee Money na kusema yafuatayo:
“Vanessamdee Sijui ulipo anzia, but mpaka apa ulipofikia umepambana sana. Nina imani mungu ndo aliye kufanyia wepesi mpaka kua #BrandKubwa na kupata hatua Ulizo nazo. Naamini Mungu Huyu Huyu ndiye atakae kufanyia Wepesi Kwenye yanayo kukabili ivi sasa. Amini izi ni Changa moto tu na ni Mapito ambayo Binadamu tunapitia kwenye Safari ya kuelekea kutimiza Ndoto zetu.
I pray for you my friend Vanessa, naamini brand yako haiwezi haribika kirahisi kwa sababu umepambana sana ni wasichana wachache wenye kuweza ku-fight kama wewe. Mungu ata kusimamia uzidi kusonga mbele, Haya yata pita nina imani utakua strongZaidi. #CashMadame KeepItUp. Napenda kuona Wasichana wakifanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii #VannesaTheBrand wewe ni mwanamke wa shoka. Usiyumbishwe kuwa Mfano. Najivunia uwepo wako kwenye Game ya Muziki wetu… Don’t give up. #VanessaTheBrand.” – Nay.
Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.