×

BREAKING NEWS: Tazama Bomoabomoa Inavyopitia Nyumba 200 za Wakazi wa Buguruni, Dar


Wakazi wa maeneo ya Buguruni na maeneo mengine wilayani Ilala, waliojenganyumba zao pembezoni mwa reli ya kati (TRL), leo tar. 11/03/2017 wameionja joto ya jiwe baada ya nyumba zilizokuwa ndani ya umbali wa mita 30 kutoka kwenye reli, zipatazo 200 kuanza kubomolewa kwa amri ya serikali.


Global Tv Online ilifika eneo la tukio na kushuhudia jinsi nyumba hizo zilivyokuwa zikibomolewa, huku wananchi wengi waliokumbwa na patashika hiyo, wakiililia serikali yao, kwani hawakupewa hata muda wa kuhamisha chochote kutoka kwenye nyumba zao.


Jeshi la polisi lilikuwepo eneo la tukio ambapo askari waliojihami kwa bunduki na mabomu ya kutoa machozi, walikuwa wakirandaranda huku na kule, kuhakikisha hakuna anayejitokeza kupinga zoezi hilo.
Tazama video kuona jinsi bomoabomoa hiyo ilivyokuwa.