
MSANII wa Bongo Fleva, Frank Mgogosi mkazi wa Kimara jijini Dar jana ameibuka Mshindi wa Shindano la Wikienda Music Search (WMS) lililoandaliwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda la ‘Unataka Kuwa Msanii Mkubwa wa Muziki’.

Fainali ya shindano hili lilifanyika kwenye Studio za Wanene Entertainment zilizopo Mikocheni jijini Dar chini ya maproduzya watano akiwemo King Luffa, Dk, Reggy, Goncher, Humphrey kutoka zimbambwe na Shente Murozy wa Studio za Black za Magomeni Kagera jijini Dar.

Akizungumza na GPL, Mgogosi ambaye ni mshindi ameyapongeza Magazeti ya Global Publishers kwa kutoa fursa mbalimbali kwa wasomaji na wasanii na kuwahimiza Watanzania kuwa na utamaduni wa kujisomea.

“Sikutegemea kama naweza kuwa mshindi maana hata mpinzani wangu Allen Venance yuko vizuri lakini kwa kuwa mshindi alipaswa awe mmoja, nimepita mimi.

“Niwashauri tu Watanzania na hasa vijana wajenge utamaduni wa kujisomea hasa Magazeti ya Global kwani kuna habari zingine ambazo zinaweza kuwa fursa kwako, alisema Mgogosi.

Aidha Mratibu wa Shindano la Wikienda Music Search (WMS), Gabriel Ng’osha amewapongeza wasanii zaidi ya 60 waliojitokeza kwa jiji la Dar e s Salaam na kuwataka kuendelea kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda, kwani limejipanga kuboresha zaidi Shindano hilo.






Na mwandishi wetu/GPL