


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Samia Suluhu na Spika Mstaafu wa Bunge la Awamu ya Nne, Anne Makinda, wamefika nyumbani kwa Marehemu George Kahama kwa ajili ya kutoa pole kwa wafiwa.

Marehemu George Kahama enzi za uhai wake alikuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe. Aidha mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business leo hii saa 11 jioni na kukesha hadi asubuhi.

Kesho mwili wa marehemu utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa mbili kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saa tano nanusu 5.30 asubuhi kwa ibada.

Ibada ya mazishi itafanyika katika makaburi ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu 9.30 alasiri.
