
Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA| MAMTONI
MWANAMITINDO Blac Chyna amekuwa mkali kwa wifi yake, Kylie Jenner kwa kumpiga stop kuwa karibu na mwanaye, King Cairo ambaye amekuwa akimlea kutokana na uhusiano wake na Tyga.
Kisa cha Blac kuamua hivyo ni baada ya kuona Kylie amekuwa akiingilia ugomvi wake na aliyekuwa mpenzi wake Rob Kardashian juu ya mtoto wao Dream Kardashian.

Mtu wa karibu na Blac alisema kuwa, kwa sasa hamuamini tena Kylie kutokana na kumtolea maneno machafu na hivyo ni baada ya kuona Kylie amekuwa akiingilia ugomvi wake na aliyekuwa mpenzi wake Rob Kardashian juu ya mtoto wao Dream Kardashian, alisema kuwa, kwa sasa hamuamini tena Kylie kutokana na kumtolea maneno machafu na kuona amedai kuwa watoto wote wawili (Dream na King) ni wa kwake na hakuna Kardashian yeyote atakayewachukua.

Blac na Tyga wamezaa mtoto mmoja, King na baada ya kuachana, Blac alianzisha uhusiano na mdogo wa Kim Kardashian, Rob na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Dream.