
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameipiga tafu Shule ya Msingi Mji mwema iliyopo Wilaya ya Kigamboni kwa kuchangia saruji mifuko 100 na mabati 100 kwa ajili ya upanuzi wa vyumba vya madarasa ya shule hiyo.

Hafla ya uchangiaji wa mifuko hiyo, ulifanyika katika shule hiyo ambapo pia kulihudhuriwa na diwani wa kata, Celestine Maufu, walimu,wadau na wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, ambao walionekana kufurahishwa na namna meya alivyojitolea kufanikisha ujenzi.

Hafla hiyo ilikuwa ya harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya upanuzi wa vyumba vya madarasa, ambapo katika hotuba yake mwenyekiti wa kamati ya shule alisema kuwa madawati yapo lakini tatizo ni sehemu ya kuyaweka.



NA DENIS MTIMA/GPL