×

Meya Dar Kuhudhuria Mkutano wa Serikali za Mitaa ‘Sauzi’

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Stori: Denis Mtima/GPL

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, leo ameondoka nchini kwenda kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa shirikisho la serikali za mitaa duniani ( ICLEI ) utakaofanyika nchini Afrika Kusini kesho na atarejea nchini Machi 25 mwaka huu.

Mkutano huo unatarajiwa kuhusisha mameya wote wa Afrika na utajikita kushugulikia mabadiliko ya tabia ya nchi na kuhakikisha matumizi mazuri ya utumiaji wa rasilimali za nchi husika.

Akizungumza na mwandishi wetu, Mwita alisema kuwa katika mkutano huo kutajadiliwa hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kujikita zaidi katika kujikinga na majanga ya mafuriko na kutafuta suluhisho la matatizo ya maji kwenye majiji.

Alisema kuwa Katika suala la maji atatumia mkutano huo kuwasilisha mada inayohusiana na kuondokana na tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam kupitia vyanzo vya maji ukiwemo Mto Ruvu, Kimbiji na vyanzo vingine.

Aidha kwa upande wa suala zima la mafuriko alisema pia atawasilisha mada kuhusiana na mafuriko na kujengewa uwezo katika kuendesha majiji yao sambamba na kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza. Pia anategemea mkutano huo kuwanufaisha wakazi wa jiji lake na mambo ambayo atakuwa ameyapata kwa kupitiafursa ya mkutano huo ili wakazi wa jiji hilo waweze kuondanokana na changamoto hiyo.