×

Basata ‘Waupiga Pini’ Wimbo wa Ney wa Mitego, Atakaeusambaza Kukiona

Na Walusanga Ndaki/GPL

BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa msanii mkali wa kuchana, Ney wa Mitego, unaoitwa

Wapo. Wimbo huo ambao ni mpya na unadaiwa kuwa na maneno yasiyo na maadili kwa jamii.

Mbali ya kuufungia wimbo huo pia Basata wamepiga marufuku kusambaza na kusikiliza nyimbo zote zilizofungiwa kuwa ni kosa kisheria.

Msanii huyo bado anashikiliwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam kutokana na wimbo wake huo.

BASATA linawaasa wasanii kutunga nyimbo zenye maadili kwa jamii.