×

Sababu za Kifo cha Faru John Zatajwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

DAR ES SALAAM: Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuchunguza kifo cha faru maarufu aliyejulikana kwa jina la Faru dume imekabidhi ripoti yake leo kwa kiongozi huyo wa serikali na kutaja sababu za kifo chake.

Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Samweli Manyele akikabidhi ripoti kwa Waziri Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alikabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Samweli Manyele na akasema kwamba sampuli zake zilipelekwa Afrika Kusini kwa uchunguzi.

Meza kuu ilivyoonekana.
Waziri mkuu akionyesha repoti kwa wanahabari.
Wanahabari na wageni waalikwa.

Katika ripoti hiyo sababu za kifo cha Faru John zimetajwa kuwa ni kukosa matunzo na uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea ya kutofuata utaratibu wa kisheria, mapungufu ya kiuongozi kwa wizara na taasisi zake.

Na Denis Mtima/GPL

CHEKI VIDEO