×

Paraguay: Waandamanaji Wamelichoma Moto Jengo la Bunge Lao

PARAGUAY: Waandamanaji nchini Paraguay, wamevamia jengo ya bunge la nchi hiyo na kulichoma moto wakipinga hatua ya bunge la senate la nchi hiyo kukutana kwa faragha, kupiga kura ya siri na kupitisha mswada wa kufanyia marekebisho kipengee cha katiba ya nchi hiyo, kitakachomruhusu Rais Horacio Cartes kuwania muhula wa pili madarakani.

 

Watu kadhaa wamejeruhiwa wakati Polisi walipofyatua risasi za mipira na michirizi ya maji ya kasi kujaribu kuwatawanya waandamanaji ili kuzima ghasia hizo. Waandamanaji hao wanasema mabadiliko hayo yanaharibu misingi na taasisi za kidemokrasia nchini Paraguay.

 

Hata hivyo Mswada huo huenda ukafanikiwa, kwani sasa unapelekwa katika bunge la daraja la pili ambako Rais Cartes ana idadi kubwa ya wabunge kutoka chama chake.

Mwaka 1992, sheria ilipitishwa kuzuia marais wa Paraguay kuwania muhula wa pili kama suhulu la kukabiliana uditeta na marais kung’angania madaraka.