×

Serikali Yapokea Msaada wa 490bn/= Kutoka Umoja wa Ulaya

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

SERIKALI ya Tanzania leo imepokea msaada wa fedha kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) wenye thamani ya Sh. bilioni 490 kwa ajili ya kuboresha huduma za kijami.

Msaada huo umekabidhiwa leo na mwenyekiti wa umoja huo anayeshughulikia huduma za maendeleo ya kijamii na uchumi, Roeland Van de Geer , ambaye alisema kuwa sababu ya utoaji msaada huo ni kutokana na kuvutiwa na uongozi wa Rais John Magufuli kuhusiana na uendeshaji wa sera za kiuchumi na umakini.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Doto James (Kustoto) akisoma hotuba yake.

Alisema msaada huo usiokuwa na masharti utafanyiwa utekelezaji bora katika mwaka wa bajeti unaoanza wa 2017/18.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Dotto James,  amesema anaushukuru umoja  huo kwa msaada huo na akawahakikishia kwamba msaada huo utaelekezwa katika huduma za kijamii  kama ilivyoelekezwa katika mkataba wao hasa katika masuala ya elimu, kilimo na sekta nyingine.

Viongozi hao wakikabidhiana mkataba.

Msaada huo utagawanywa katika awamu nne ambapo kila mwaka wa fedha kitatolewa kiasi cha Sh. billion 120 cha fedha hizo.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Denis Mtima/GPL